Wasifu

TP. Lucas A. Mwaisaka

Msajili, Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji

Maelezo ya Kibinafsi

Mahali alipozaliwa: Kyela, Mbeya

Tarehe ya Kuzaliwa: Julai 8, 1965

Hali ya ndoa: Ameoa na ana watoto watatu.

Uraia: Mtanzania

Anwani ya Mawasiliano: S.L.P 77496 Dar es Salaam

Barua Pepe: mwai2005@yahoo.co.uk

Simu: +255 784 260266

Elimu na Mafunzo

TP Lucas Aron Mwaisaka alipata elimu yake ya Msingi katika shule ya Msingi Mbala na kuhitimu mwaka 1981.

Alipata elimu yake ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Mbeya {Mbeya Secondary School) kati ya mwaka 1982 hadi 1985. Mwaka 1986 hadi 1988 alisoma elimu ya kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari ya Tosamaganga Iringa.

Mwaka 1989 alijiunga na Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es salaam ambako alihitimu mwaka 1992, akisomea Stashahada ya Juu ya mipango miji na vijijini. (URP).

Mwezi Disemba 2001, alijiunga na Chuo cha Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam ambako alipata Astashahada ya Uzamili katika fani ya Mipangomiji na Mazingira. (Postgraduate Certificate in Environment Management and Planning).

Katika kipindi cha Mwaka2003- 2004 alipata mafunzo ya Shahada ya Uzamili katika fani ya Mipangomiji na Usimamizi wa miji (Urban Planning and Management)katika chuo Kikuu cha Twente kitivo cha ITC – Enschede Uholanzi.

Katika kipindi cha mwezi Mei na Juni 2010 alijunga na Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo cha Weitz kilichopo Rehovot Israel (Hebrew University of Jerusalem) kupata Astashahada ya Uzamili ya Mipangomiji kuhusu Uboreshwaji wa Makazi duni (Slums Upgrading and Provision of Services to the Urban Poor).

Mafunzo mengine mbalimbali aliyahudhuria ni pamoja na Participatory GIS and Participatory Mapping in Resource Management and Conflict Mitigation yaliyotolewa naChuo kikuu cha Twente kwa kushirikiana na ERMIS Africa yaliyofanyika Mwezi Agosti na Septemba 2005 Nairobi nchini Kenya.Aidha,mwaka 2006 alipata mafunzo kuhusu Ecosystems modeling and Scenario Development for Environmental Management katika Chuo Kikuu cha Namibia (Namibia University of Science and Technology) kilichopo Windhoeck,

Mnamo Mwezi Septemba 2008 alihudhuria mafunzo kuhusu Decision Support Systems for Sustainable Urban Development in Eastern Africa yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala Uganda. Katika kujiendeleza na mafunzo, mnamo mwezi Julai 2009 alihudhuria mafunzo kuhusu Environmental Waste Management katika Taasisi ya Mafunzo na Utafiti ya Umoja wa Mataifa (United Nations institute for Training and Research) yaliyofanyika Durban Afrika ya Kusini.

Aidha,mwezi Novemba 2010, TP. Mwaisaka alipata mafunzo kuhusu Participatory Approaches to Slums Upgradingand Managemet yaliyoendeshwa na Chuo Kikuu cha Twente huko Kisumu, Kenya.

Halikadhalika mwaka 2012 alienda Jiji la Maputo,Msumbiji katika mafunzo kuhusu Research and Innovation for Rural Mobility and Access in Africa yaliyotolewa na Idara ya Kimataifa Maendeleo ya Uingereza (DFID).

Mwezi Disemba 2013 alipata mafunzo kuhusu Communuty - Based Risk Assessment and Strategy Development yaliyotolewa na Chuo Kikuu cha Makerere Kampala Uganda na kumalizia na mafunzo kuhusu Project Management katika Chuo Kikuu cha China cha kilimo kilichoko Beijing China, Mnamo mwezi Oktoba 2014.

Tp, Mwaisaka amehudhuria mafunzo mbalimbali ndani ya nchi kuhusu masuala ya Maendeleo ya miji pamoja na Usimamizi wa Mazingira yaliyotolewa wakati na sehemu mbalimbali.nchini.

Uzoefu Ndani ya Serikali

TP Mwaisaka aliteuliwa Kuwa Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji Mnamo mwezi Juni 2021. Kabla ya wadhifa huu, amefanya kazi katika Ofisi ya Rais TAMISEMI kati ya mwaka 1992 hadi 2020, pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika kipindi cha mwaka Mmoja.

Katika ofisi ya Rais TAMISEMI amefanya kazi katika nafasi mbalimbali ambapo kwa kuanzia, aliajiriwa mwaka 1992 kama Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji ambapo alitumikia Cheo hicho hadi mwaka 1994.

Ilipofika mwaka 1994 aliazimwa na kufanya kazi katika Mradi wa Umeme wa Gesi wa Songosongo (Songosongo Gas –to- Electricity Project) kama Afisa Mipango Miji akisimamiwa na Chuo Kikuu cha Ardhi hadi mwaka 1997.

Kati ya mwaka 1998 na 2007 alifanya kazi kama Afisa Mipangomiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. Ilipofika mwaka 2008, alihamishiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambako alikaimu nafasi ya Mkuu wa Idara ya Ardhi na Usimamizi wa Mazingira, hadi mwaka 2010.

Kati ya mwaka 2011 hadi 2012 aliazimwa kama Mtaalamu Mshauri katika masuala ya ardhi kwenye Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Dar es Salaam kwenye Mradi wa Local Integration Programme uliokuwa unasimamiwa na OR TAMISEMI.

Ilipofika mwezi machi 2012 aliteuliwa kuwa Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Morogoro aliyekuwa anashugulikia Idara ya Miundombinu ambako alifanya kazi hadi mwezi Septemba 2019, alipohamishiwa katika Ofisi ya |Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuendelea na wadhifa wa Katibu Tawala Msaidizi hadi Machi 2020.

Kati ya mwezi Aprili 2020 hadi Mei 2021 alifanya kazi kama Afisa Mipangomiji wa Mkoa wa Dar es Salaam hadi alipopata uteuzi wa kuwa Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji mnamo mwezi Juni, 2021.

TP. Mwaisaka ni mjumbe katika Taasisi zifuatazo:

1.International Forum for Participatory GIS,

2.ITC Alumni Association, Uholanzi,

3.The Rehovot Approach of Integrated Development, Israeli.

4. The Weitz Centre Friends’ Network, Israeli

5.Town Planners Registration Board, Tanzania.