TANGAZO KWA UMMA
Tunapenda kuziarifu Mamlaka zote za Upangaji Miji (Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya) pamoja na Umma kwa ujumla, kuwa Kampuni zilizotajwa hapa chini ambazo zinajishughulisha na kazi za Upangaji Miji (Town Planning Consulting Firms), kuwa zimefutiwa Usajili wake na Bodi kuanzia tarehe 15 Mwezi Januari Mwaka 2025.
- 1.Savei Consult Limited S.L.P 22272 DAR ES SALAAM
- 2.Summit Land Planners (T) Limited S. L. P 175 DAR ES SALAAM
- 3.Ninze Ardhi Company Limited S. L. P 552 DAR ES SALAAM
- 4.Maxima Lands Company Ltd S. L. P 14894 DAR ES SALAAM
- 5.D & J Land and Development Services S. L. P 24524 DAR ES SALAAM
Hivyo basi, Kampuni hizi haziruhusiwi kufanya kazi zozote zile zinazohusiana na Mipango Miji. Aidha, Kampuni, Mashirika na Umma kwa ujumla, unashauriwa kutokuingia au kuendelea kutekeleza mikataba yeyote inayohusiana na kazi za Mipangomiji na Kampuni hizi. Kufanya hivyo itakuwa kinyume na kifungu cha 22 na 23 cha Sheria ya Kusajili Wataalam wa Mipangomiji, Sheria Na. 7 ya Mwaka 2007. Bodi haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu au Kampuni yeyote ambayo itakiuka sheria hii.
MSAJILI
TPRB.