TAARIFA KWA UMMA

News Image Jan, 09 2026

Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) anawakumbusha Wataalamu na Kampuni za mipangomiji ambazo bado hazijalipa ada ya mwaka (Annual Fee) kulipa ili kuhuisha leseni zao kwa mujibu wa Kanuni ya 9 ya Kanuni za Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji, GN. 174 ya 2018.

Mtaalamu au Kampuni yoyote ya Mipangomiji ambayo haijahuisha leseni ya kufanya kazi za Mipangomiji kwa mwaka 2026 hadi sasa, hairuhusiwi kufanya kazi yoyote ya Mipangomiji, hadi mtaalamu au kampuni hiyo itakapolipia ada ya mwaka na kupata leseni.

Bodi itachukua hatua za kisheria ikiwemo kuwafutia usajili Wataalam na Kampuni ambazo zinafanya kazi bila kuhuisha leseni zao.

Imetolewa na:

MSAJILI

BODI YA USAJILI WA WATALAAM WA MIPANGOMIJI