TANGAZO
Dec, 24 2025
Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) inapenda kuwakumbusha wataalamu na kampuni za mipangomiji zilizosajiliwa kutoa taarifa kwa Bodi kuhusu mabadiliko ya anwani ya makazi, anwani ya posta, anwani ya barua pepe, namba ya simu kama ilivyoelekezwa katika Kanuni ya 26(3) ya Kanuni za Usajili wa Wataalam wa Mipangomiiji za 2018. Kanuni hii inamtaka mtaalamu au Kampuni ya mipangomiji kuijulisha Bodi kuhusu mabadiliko ya anwani ndani ya siku 30 tangu kufanyika kwa mabadiliko hayo.
Mtaalamu au Kampuni husika inatakiwa kujaza fomu Na. TPR 7 ya kubadilisha anuani inayopatikana kwenye tovuti rasmi ya Bodi www.tprb.go.tz kupitia kiunganishi https://www.tprb.go.tz/uploads/publications/en1766466863-FOMU%20MAOMBI.pdf na kutumwa kwa Msajili kupitia registrar@tprb.go.tz kabla au ifikapo tarehe 22 Januari, 2026.
Mtaalamu au Kampuni ambayo haitawasilisha mabadiliko ya taarifa zake ndani ya muda huo itakabiliwa na hatua za kisheria kwa mujibu wa Kanuni ya 26(3) ya Kanuni za Usajili wa Wataalam wa Mipangomiiji za 2018, zikisomwa pamoja na Jedwali la pili la kanuni hizo.
Wataalamu na Kampuni zote za mipangomiji zinahimizwa kuzingatia tangazo hili.
Imetolewa na:
TP. Martha Mkupasi
KAIMU MSAJILI
23/12/2025


