MAHITAJI YA USAJILI
MAHITAJI YA USAJILI
A. USAJILI WA MTU BINAFSI
1.Mwombaji awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu (3) wa vitendo kama Mtaalamu wa Mipangomiji.
2.Kitambulisho cha uraia
3.Kazi tatu (3) za Mipangomiji zilizoidhinishwa pamoja na taarifa zake za kitaalamu (planning briefs).
4.Fomu ya Maombi ya Usajili (nakala mbili) – inapatikana katika tovuti ya TPRB: http://www.tprb.go.tz.
5.Vyeti vya taaluma (Chuo Kikuu, Kidato cha 6 na Kidato cha 4) pamoja na cheti cha matokeo (transcript) ya Chuo Kikuu.
6.Wasifu wa sasa wa mtaalam (CV).
7.Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN).
8.Picha mbili (2) za rangi (pasipoti)
9.Risiti ya ada ya usajili:
a)Sh. 100,000 kwa raia wa Tanzania.
b)Dola 1,500 kwa wasio raia.
B. USAJILI WA KAMPUNI
1.Maafisa Mipangomiji wawili (2) wenye usajili kamili, ambapo mmoja wao ni Mkurugenzi na mmiliki mwenye hisa nyingi, au Maafisa Mipangomiji wawili wenye usajili kamili Pamoja na kumiliki hisa zaidi ya asilimia 50.
2.Nakala ya vyeti vya usajili kwa Maafisa mipangomiji ambao ni Wakurugenzi.
3.Picha mbili (2) za rangi za wakurugenzi (pasipoti) za hivi karibuni.
4.Wasifu wa sasa wa wakurugenzi (CV).
5.Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN).
6.Leseni ya biashara iliyotolewa na mamlaka husika.
7.Cheti cha usajili wa kampuni kutoka mamlaka husika
8.Fomu ya Maombi ya Usajili (nakala mbili) – inapatikana katika tovuti ya TPRB: http://www.tprb.go.tz.
9.Wasifu wa sasa wa kampuni (Company Profile).
10.Katiba na Kanuni za Kampuni (Memorandum & Articles of Association) - zioneshe kuwa kazi kuu ya kampuni ni kazi za upangaji miji.
11.Uthibitisho wa kuwa na ofisi ya kazi za mipangomiji.
12.Risiti ya ada ya usajili:
a)Sh.350,000 kwa kampuni za ndani.
b)Dola 2,200 kwa kampuni za kigeni.
13.Masharti ya ziada kwa kampuni za kigeni:
a) Uthibitisho wa usajili katika nchi ya asili kabla ya kuja Tanzania.
b) Uthibitisho wa kuteuliwa kufanya kazi ya Mipango miji nchini Tanzania.
c) Kibali cha kazi nchini kutoka mamlaka husika.
d) Uthibitisho wa kushirikiana na kampuni ya ndani ya Mipango miji iliyosajiliwa.
e) Katiba ya kampuni ioneshe kuwa kazi kuu ni Mipango miji.
f) Kiapo kinachoonesha kuwa usajili utasitishwa mara baada ya kazi ya mipangomiji aliyoteuliwa kufanya kukamilika.
TANBIHI
ØMalipo yote yafanywe kupitia Namba ya Malipo ya Serikali (Control Number) inayopatikana katika mfumo wa Ankara wa bodi: https://billing.tprb.go.tz.
Ø Kwa mawasiliano zaidi:
Simu: +255 (026) 232 3833 | +255 739 504 222
Baruapepe: registrar@tprb.go.tz
Tovuti: www.tprb.go.tz
ØMaombi ya usajili wa kampuni ya mipangomiji yaliyofanywa na mtaalamu mwenye usajili kamili lakini ana deni la ada ya mwaka hayatashughulikiwa hadi atakapolipa deni hilo.