WATUMISHI WA TPRB WASHIRIKI KAMPENI YA KITAIFA YA UPANDAJI MITI KUIMARISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA
Jan, 28 2026
Watumishi wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) wameungana na Watanzania wengine katika kampeni maalumu ya kitaifa ya upandaji miti, ikiwa ni sehemu ya mkakati ya kuhifadhi mazingira na kumtakia heri ya Siku ya Kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Zoezi hilo limefanyika Jumanne, Januari 27, 2026, katika Ofisi za TPRB zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, ambapo watumishi walipanda miti mbalimbali ikiwa ni mkakati wa kuhifadhi na kulinda mazingira ikiwa ni kutekeleza kauli mbiu ya ‘‘ Uzalendo ni Kutunza Mazingira, Shiriki Kupanda Miti''
Hii ni miongoni mwa jitihada inazofanya TPRB kuendeleza ajenda ya ulinzi wa mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.
Kampeni hiyo ya upandaji miti ni sehemu ya kuunga mkono maono ya Rais Samia ya kulinda na kuhifadhi mazingira ikiwa inaakisi upangaji miji endelevu unaoendana na uhifadhi wa mazingira na rasilimali asilia, ambapo kabla ya watumishi wa TPRB kushiriki zoezi hilo lilizinduliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo na Naibu wake Mhe. Kaspar Mmuya kwenye Ofisi za Wizara zilizopo eneo la Mtumba jijini Dodoma


