LICENSE RENEWAL
TANGAZO LA KUHUISHA LESENI
Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji inawakumbusha wataalam na kampuni zote zilizosajiliwa kuhuisha leseni zao kwa mujibu wa Kanuni ya 9 ya Kanuni za Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji, Tangazo la Serikali Na. 174 la mwaka 2018. Leseni ya kufanya kazi za Mipangomiji ni ya muda wa Mwaka mmoja kuanzia tarehe 01 Januari hadi tarehe 31 Disemba kila Mwaka.
Wataalamu na Kampuni zilizosajiliwa zinatakiwa kuhusisha leseni zao kwa kulipa Ada ya Mwaka kama ilivyelekezwa katika Kanuni ya 8 ya Kanuni za Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji, Tangazo la Serikali Na. 174 la mwaka 2018, zikisomwa pamoja na jedwali la kwanza la kanuni tajwa hapo juu.
Mtaalam au Kampuni yoyote ya Mipangomiji ambayo haitahuisha leseni ya kufanya kazi za Mipangomiji kwa mwaka 2026 hadi kufikia tarehe 01/01/2026, haitaruhusiwa kufanya kazi za Mipangomiji. Aidha, Bodi itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za Sheria ikiwemo kuwafutia usajili Wataalam na Kampuni ambazo zitashindwa kulipa Ada ya Mwaka ili kuhuisha leseni zao kwa wakati.
Imetolewa na:
MSAJILI
BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI
8-Disemba 2025.


