TAARIFA KWA UMMA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI
TAARIFA KWA UMMA
KUHAMA OFISI ZA BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI
Dodoma, Septemba 18, 2025.
Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji Sura ya 426 ili kusimamia taaluma ya Mipangomiji na utendaji kazi wa Wataalamu wa Mipangomiji na Kampuni zinazofanya kazi za mipangomiji pamoja na kuishauri Serikali masuala mbalimbali yanayohusu taaluma ya mipangomiji nchini.
Bodi inapenda kuwataarifu wataalam wa Mipangomiji, wananchi, wadau wa sekta ya mipangomiji, na umma kwa ujumla kuwa kuanzia tarehe 17/09/2025 imehamisha rasmi ofisi kutoka eneo la Sabasaba ilipokuwa awali na sasa zinapatikana Mji wa Serikali Mtumba, jengo dogo la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Hivyo wadau wote mnakaribishwa katika ofisi mpya za Bodi kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi.
Imetolewa na;
Msajili
BODI YA USAJILI WA WATALAAM WA MIPANGOMIJI