KUWASILISHA TAARIFA YA KAZI ZA MIPANGOMIJI

News Image Feb, 20 2025

TAARIFA YA KAZI ZA KITAALAM ZINAZOTEKELEZWA NA KAMPUNI PAMOJA NA WATAALAM WA MIPANGOMIJI WALIOSAJILIWA

Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.

2.Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa sheria ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji Na. 7 ya mwaka 2007 ili kusimamia taaluma ya Mipangomiji pamoja na utendaji kazi wa wataalam wa Mipangomiji na Kampuni zinazofanya kazi za mipangomiji.

3.Kifungu cha 14 cha sheria ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji Na. 7 ya mwaka 2007 kinampa Msajili wajibu wa kupata taarifa kutoka kwa wataalam wa mipangomiji waliosajiliwa. Wataalam wa Mipangomiji mliosajiliwa pamoja na Kampuni za Mipangomiji, mnatakiwa kuwasilisha taarifa za kazi za kitaalam mnazozifanya kila mwaka.

Aidha, Kifungu cha 24 cha marekebisho ya sheria mbalimbali Na.4A ya mwaka 2017

( miscellaneus Ammendment Act. No. 4A of 2017) kilirekebisha kifungu cha 2 cha sheria ya usajili wa wataalam wa mipangomiji Na. 7 ya mwaka 2007 na kutoa orodha ya makundi ya kazi za mipangomiji, hivyo kazi au miradi itakayowasilishwa izingatie kazi za mipangomji zinazotambuliwa na sheria tajwa hapo juu.

4.Taarifa za kazi zilizotekelezwa na kampuni pamoja na wataalam zinapaswa kuwasilishwa kati ya tarehe 01 hadi 20 ya mwezi Julai kila mwaka, zikijumuisha kazi zote za kitaalam na miradi iliyotekelezwa.

Hata hivyo hadi kufikia Disemba, 2024 hakuna taarifa zilizopokelewa toka kwa mtaalam binafsi au kampuni.

5. Kwa barua hii mnatakiwa kuwasilisha taarifa ya mwaka 2023/2024 kabla ya tarehe 15/03/2025 kwa kuzingatia muundo ulioonyeshwa kwenye jedwali lililooambatishwa na barua hii.

Nawatakia utekelezaji mwema.

TP. Lucas A. Mwaisaka

MSAJILI