TANGAZO LA KUSAJILI WATAALAM WA MIPANGOMIJI NA KAMPUNI ZA UPANGAJIMIJI

News Image Jan, 04 2025

TANGAZO LA KUSAJILI WATAALAM WA MIPANGOMIJI NA KAMPUNI ZA UPANGAJIMIJI

Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji inawatangazia Watalaam wa Mipangomiji wote wenye sifa ya kusajiliwa na ambao bado hawajasajiliwa kuwa Bodi inategemea kufanya kikao cha kusajili watalaam wa Mipamgomiji na Kampuni za Upangaji Miji mwishoni mwa mwezi Januari, 2025.

Bodi inapokea maombi kwa ajili ya usajili na mwisho wa kupokea maombi hayo ni siku ya Jumanne tarehe 19/01/2025, maombi yote yawasilishwe Ofisi ya Msajili, S. L. P. 1150, 41102 DODOMA. Simu: +255 (026) 232 3833, +255 739 504 222.

Kwa taarifa zaidi ingia kwenye tovuti ya Bodi ya Usajili wa Watalaam wa Mipangomiji- www.tprb.go.tz