ALERT

Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji inawajulisha Wataalam wote wa mipangomiji ambao ni waajiriwa serikalini na wamelimbikiza madeni yao ya ada za mwaka kuhakikisha wanalipa madeni yao kabla ya tarehe 30/09/2024.Baada ya tarehe hiyo Bodi itachukua hatua za kisheria kudai madeni hayo.Hivyo unatakiwa kulipa deni kwa mujibu wa Kanuni za Sheria ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji za Mwaka 2018 Kifungu cha 8(1) -(5).

Aidha, Bodi inatoa muda wa miezi miwili kwa Wataalam ambao hawajasajiliwa kuhakikisha wanajisajili.Baada ya muda huo kupita hakuna Mtaalam yeyote atakayeruhusiwa kutekeleza kazi zozote za taaluma ya mipangomiji bila kusajiliwa na Bodi, kama inavyobainishwa kupitia Kifungu cha 22 cha Sheria ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji Na.7 ya Mwaka 2007 pamoja na marekebisho yake.

TP. Lucas A. Mwaisaka

MSAJILI

19 Agosti, 2024