TANGAZO KWA MAAFISA MIPANGOMIJI MAANDIKO YA MADA ZA MKUTNO MKUU WA 11 WA MWAKA WA MAAFISA MIPANGOMIJI

Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji inawakaribisha Wataalamu wa Mipangomiji

wenye nia ya kuwasilisha mada katika mkutano mkuu wa mwaka wa Wataalamu wa

Mipangomiji, kuwasilisha maandiko (papers) zitakazowasilishwa katika Mkutano huo

utakaofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Oktoba 2026, Jijini Arusha.

Maandiko yatakayowasilishwa yanapaswa kuendana na kaulimbiu ya mkutano huo

ambayo ni: “Mabadiliko ya Kidijitali katika Mipangomiji kwa Udhibiti Bora wa Ukuaji wa

Miji” (Digital Transformation of Urban Planning Practice for Effective Physical

Development Control). Maandiko yote yawasilishwe kwa Msajili wa Bodi kupitia barua

pepe registrar@tprb.go.tz. Bodi itawasiliana na wataalamu ambao Maandiko

waliyowasilisha yamechaguliwa kwa ajili ya uwasilishaji. Mwisho wa kuwasilisha

maandiko ni tarehe 18 Septemba 2026 saa 9:30 Alasiri.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Ofisi ya Msajili kwa namba +255 739 504 222 au TP.

Aloyce Massaga kwa namba 0765273090.

Imetolewa na;

TP. Martha Mkupasi

Kaimu Msajili