TANGAZO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI

TANGAZO

Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB), inapenda kuutarifu umma kwamba, kufuatia marekebisho ya Sheria ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji Sura ya 426, yaliyotangazwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 12 la tarehe 1 Desemba, 2023, (The Written Laws (miscellaneous Amendments (No.4) Act 2003 Part X), inaelekezwa kwamba kazi zote zinazohusiana na taaluma ya Mipangomiji zitakazofanywa kupitia Mamlaka za Upangaji, Kampuni binafsi za Upangaji pamoja na Wataalam wa mipangomiji waliosajiliwa, zinatakiwa kusajiliwa na Bodi kupitia Mfumo wake wa TPRB Billing System.

Hatua hii itaiwezesha Bodi, kuimarisha ufuatiliaji wa kazi zote za kitaaluma zinazofanyika nchini, kuwa na kanzidata ya kazi hizo pamoja na kuimarisha mapato ya Serikali.

Kupitia tangazo hili, Mamlaka za Upangaji, Kampuni za mipangomiji na wataalam waliosajiliwa mnakumbushwa wajibu wa kuanza kusajili Miradi yote inayotegemewa kutekelezwa kuanzia sasa kwenye Mfumo wetu iliounganishwa na Mfumo wa ILMIS wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi utakaowezesha kufanyika kwa uidhinishaji wa kazi zote za miradi hiyo kijiditali.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea tovuti yetu rasmi ya www.tprb.go.tz au wasiliana nasi kupitia simu Na. 0739 504 222au Barua pepe: registrar@tprb.go.tz .

Limetolewa na:

MSAJILI

BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI