TANGAZO!! UTARATIBU WA UTOAJI TUZO YA UMAHIRI KATIKA TAALUMA YA MIPANGOMIJI

Bodi ya Usajili wa Wataalan wa Mipangomiji inapenda kuwatangazia wataalam wa Mipangomiji kuwa utoaji wa tuzo za umahiri katika utendaji kazi za Mipangomiji kwa mwaka 2022/2023 utafanyika katika Mkutano Mkuu wa Nane wa Mwaka unaotarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 24/10/2022 hadi tarehe 25/10/2022.

Tuzo zitakazotolewa zitakuwa katika makundi matatu kama ifuatavyo: -

i.Mtaalam binafsi aliyefanya kazi kwa ubunifu na kuleta matokeo yenye ufanisi wa pekee kwa jamii.

ii.Kampuni iliyofanya mradi au miradi kwa ufanisi Mkubwa.

iii.Mradi uliotekelezwa kwa ubunifu na ufanisi.

Wataalam wa Mipangomiji na Kampuni mnaombwa kuwasilisha andiko fupi (lisilozidi kurasa tatu) linaloelezea mradi au kazi ambayo umetekelezwa kwa ufanisi. Andiko hilo liwasilishwe kwaMsajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji kwa email registrar@tprb.go.tz au njia ya posta kwa anwani - S. L. P 1150, Dodoma kuanzia tarehe 12/08/2022 hadi tarehe 12/09/2022 Saa 9:30 Alasiri

Maandiko yatakayofanyiwa kazi ni yale tu ambayo yatawasilishwa ndani ya muda tajwa hapo juu.

Limetolewa na:

Msajili

Bodi ya Usajii wa Wataalam wa Mipangomiji

10/08/2022