USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI NA MAKAMPUNI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI
TANGAZO LA KUSAJILI WATAALAM WAMIPANGOMIJI NA KAMPUNI ZA UPANGAJI MIJI
Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji inawatangazia Watalaam wa Mipangomiji wote wenye sifa ya kusajiliwa na bado hawajasajiliwa kuwa Bodi inategemea kufanya kikao cha kusajili watalaam wa Mipangomiji na Kampuni za UpangajiMiji mwishoni mwa mwezi Disemba, 2023.
Bodi inapokea maombi kwa ajili ya usajili, mwisho wa kupokea maombi hayo ni siku ya Ijumaa tarehe 29/12/2023, maombi yote yawasilishwe Ofisi ya Msajili, S. L. P. 1150, 41102 DODOMA. Simu: +255 (026) 232 3833, +255 739 504 222.
Kwa taarifa zaidi ingia kwenye tovuti ya Bodi ya Usajili wa Watalaam wa Mipangomiji-www.tprb.go.tz
Limetolewa na:
KAIMU MSAJILI
BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI
15/11/2023
Barabara ya Maktaba, S. L. P. 1150, 41102 DODOMA. Simu: +255 (026) 232 3833,+255 753 504 222,
Tovuti: http//www.tprb.go.tz, Baruapepe: registrar@tprb.go.tz