USAJILI WATAALAM WA MIPANGOMIJI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI
TANGAZO LA KUSAJILI WATAALAM WA MIPANGOMIJI
Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji inawatangazia Watalaam wa Mipangomiji wote ambao wanasifa ya kusajiliwa na bado hawajasajiliwa kuwa Bodi inategemea kufanya kikao cha kusajili watalaam wa Mipamgomiji mwishoni mwa mwezi Januari 2023. Hivyo bodi inapokea maombi kwa ajili ya usajili,mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15/01/2023. Maombi yote yawasilishwe kwa Msajili, S. L. P. 1150, 41102 DODOMA. Simu: +255 (026) 232 3833, +255 739 504 222, Barua pepe: registrar@tprb.go.tz
Tangazo hili linapatikana pia katika tovuti ya Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji ambayo ni www.tprb.go.tz.
Limetolewa na:
TP Lucas Mwaisaka
MSAJILI
BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI
27/12/2022