MAFUNZO ENDELEVU YA KITAALUMA (CPD) KWA WATAALAMU WA MIPANGOMIJI TANZANIA BARA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGO

Wataalamu wa Mipangomiji,

TANZANIA BARA.

Kuh: MAFUNZO ENDELEVU YA KITAALUMA (CPD) KWA WATAALAMU WA MIPANGOMIJI TANZANIA BARA

Tafadhali rejea somo tajwa hapo juu.

Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji imeandaa mafunzo endelevu ya kitaaluma (CPD) kwa ajili ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Mipangomiji nchini. Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 07/06/2023 hadi tarehe 08/06/2023 katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, Jiji la Arusha kuanzia saa 2:00 Asubuhi. Mafunzo ya mwaka huu yatahusu uandaaji wa maandiko ya miradi na utafutaji wa rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Mipangomiji.

Wataalamu wa Mipangomiji waliopo katika Wizara Mbalimbali, Halmashauri, Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma, Ofisi za Ardhi za Mikoa na Sekta Binafsi mnaalikwa kuhudhuria Mafunzo hayo muhimu yatakayowaongezea weledi katika utekelezaji wa majukumu yenu.

Gharama za ushiriki kwa Mshiriki mmoja ni shilingi laki tatu (300,000/=) itakayo jumuisha gharama mbalimbali ikiwemo chakula wakati wa mafunzo, shajala pamoja na makabrasha ya mafunzo. Malazi na Usafiri vitagharamiwa na wataalamu wenyewe au Ofisi zao kwa wale walioajiriwa. Thibitisha ushiriki wako kabla au ifikapo tarehe 02/06/2023 kwa kulipia gharama ya ushiriki itakayoilipwa kupitia namba ya kumbukumu(control number) utakayopatiwa kwa kupiga namba 0739 594 222.

Ninashukuru kwa ushirikiano wenu.

TP. Lucas A. Mwaisaka

MSAJILI.