TANGAZO KWA UMMA-​UTARATIBU WA KUSAJILIWA

News Image Oct, 20 2025

UTARATIBU WA KUSAJILIWA KAMA AFISA MIPANGOMIJI ALIYEHITIMU (GRADUATE TOWN PLANNER) PAMOJA NA AFISA MIPANGOMIJI MSAIDIZI (TECHNICIAN TOWN PLANNER)

Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji, ni Taasisi ya Serikali iliyoundwa chini ya Sheria ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji Sura ya 426. Mojawapo ya jukumu la Bodi ni kusajili Wataalamu wa Mipangomiji pamoja na Kampuni zinazofanya kazi za Mipangomiji. Bodi inatekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa Kifungu cha 11C na 11D cha Sheria ya Usajili wa wataalamu wa Mipangomiji Sura ya 426 ikisomwa pamoja na Kanuni ya 4 ya Kanuni ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji, Gazeti la Serikali Namba 174 la Mwaka 2018.

Bodi inapenda kuwatangazia Wataalamu wa Mipangomiji waliohitimu Taaluma ya Mipangomiji kujisajili ili watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa Sheria, taratibu na Kanuni. Zifuatazo ni Sifa za Kusajiliwa:

A. Afisa Mipangomiji Aliyehitimu (Graduate Town Planner)

  • i.Awe Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • ii.Awe amehitimu shahada ya kwanza ya Mipangomiji katika chuo kinachotambuliwa na Serikali
  • iii.Ajaze fomu nakala 2 za maombi ya usajili
  • iv.Uthibitisho wa malipo ya Ada ya maombi ya Usajili (Tanzania shilingi) 75,000/=
  • v.Wasifu (Curriculum Vitae)
  • vi.Aambatanishe picha 2 za rangi (Current colored passport size)
  • vii.Aambatanishe vyeti vya taaluma na matokeo (Academic certificate and Transcript)

B. AFISA MIPANGOMIJI MSAIDIZI (Technician Town Planner)

  • i.Awe Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • ii.Awe amehitimu Astashahada ya Mipangomiji katika chuo kinachotambuliwa na Serikali
  • iii.Ajaze fomu nakala 2 za Maombi ya Usajili
  • iv.Uthibitisho wa malipo ya Ada ya Maombi ya Usajili Shilingi 50,000/=
  • v.Wasifu (Curriculum Vitae)
  • vi.Aambatanishe picha za rangi 2 (current colored passport size)
  • vii.Aambatanishe vyeti vya taaluma na matokeo (Academic certificate and Transcript)
  • viii.Awe amefaulu Mtihani uliotolewa na Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji

Maombi yote yatumwe kwa Barua pepe ya Msajili: registrar@tprb.go.tz au abdallah.mmenga@tprb.go.tz