USAJILI !!

News Image Oct, 01 2024

Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji inawatangazia Watalaam wa Mipangomiji wote wenye sifa ya kusajiliwa na ambao bado hawajasajiliwa kuwa Bodi inategemea kufanya kikao cha kusajili watalaam wa Mipangomiji na Kampuni za Upangaji Miji mwanzoni mwa mwezi Oktoba, 2024.

Bodi inapokea maombi kwa ajili ya usajili na mwisho wa kupokea maombi hayo ni siku ya Jumanne tarehe 10/10/2024, maombi yote yawasilishwe Ofisi ya Msajili, S. L. P. 1150, 41102 DODOMA. Simu: +255 (026) 232 3833, +255 739 504 222.

Kwa taarifa zaidi ingia kwenye tovuti ya Bodi ya Usajili wa Watalaam wa Mipangomiji- www.tprb.go.tz

Limetolewa na:

TP. Lucas A.Mwaisaka

MSAJILI

BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI

30/09/2024