KUAHIRISHWA KWA MKUTANO MKUU WA TISA WA MWAKA WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI
Oct, 01 2024Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji kwa kushirikiana na Chama cha Wataalam wa Mipangomiji Tanzania (TITP) inawataarifu wataalam wa Mipangomiji, wadau wa Mipangomiji na waalikwa wote kuwa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Mwaka uliotarajiwa kufanyika Tarehe 7-9 Oktoba, 2024 katika Jiji la Dar es Salaam umeahirishwa hadi mwanzoni mwa mwezi Novemba, 2024. Tarehe za kufanyika kwa Mkutano huo pamoja na Ukumbi mtaarifiwa hapo baadae.
Wataalam wa Mipangomiji na wadau mbalimbali ambao hamjakamilisha kuchangia ada ya ushiriki, mnaombwa kukamilisha uchangiaji.
Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji inaomba radhi kwa usumbufu wowote ambao utakuwa umejitokeza.
Tangazo hili linapatikana pia katika tovuti ya Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji ambayo ni www.tprb.go.tz
MSAJILI
BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI
30/09/2024