KUAHIRISHWA KWA MKUTANO MKUU WA NANE WA MWAKA WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI

TANGAZO LA KUAHIRISHWA KWA MKUTANO MKUU WA NANE WA MWAKA WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI

Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji kwa kushirikiana na Chama cha Wataalam wa Mipangomiji Tanzania (TITP) inawataarifu wataalam wa Mipangomiji, wadau wa Mipangomiji na waalikwa wote kuwa Mkutano Mkuu wa Nane wa Mwaka uliotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba, 2022 katika Jiji la Dodoma umeahirishwa hadi mwanzoni mwa mwezi Machi, 2023. Tarehe za kufanyika kwa Mkutano huo pamoja na Ukumbi mtaarifiwa hapo baadae.

Wataalam wa Mipangomiji na wadau mbalimbali ambao hamjakamilisha kuchangia ada ya ushiriki, mnaombwa kukamilisha uchangiaji.

Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji inaomba radhi kwa usumbufu wowote ambao utakuwa umejitokeza.


Limetolewa na:

MSAJILI

BODI YA USAJILI WA WATAALAM WA MIPANGOMIJI

30/11/2022.